Klabu ya Shabana FC ambayo msimu ujao itakuwa inashiriki katika ligi kuu ya fkf hapa nchini kwa mara ya kwanza baada ya takriban miaka 30 inalenga kumtangaza mdhamini mkuu wa shati katika sare zao hii leo wanapozidi kujenga misuli yao kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2023/2024.
Gavana wa kaunti ya Kisii Simba Arati ambaye alichaguliwa kuwa Patroni wa klabu hiyo akiwapiku Sam Nyamweya na Ezekiel Machogu katika nafasi hiyo ametangaza kuisaidia kilabu hiyo katika kutafuta wadhamini ambao watawekeza kuipa nguvu klabu hiyo.
Arati amewahimiza na kuwaomba wachezaji wa klabu hiyo wa sasa kutokubali ofa zozote za kutaka kuhamia klabu nyingine kwani katika klabu hiyo maslahi yao yatasimamiwa vilivyo.

