Bondia wa Kenya Fatuma Zarika maarufu kama Iron Fist analenga kutetea ubingwa wake wa shirikisho la ndondi ulimwengini katika mashindano ya taji la World Super Featherweight baada ya kuibuka bingwa wa taji hilo miaka miwili iliyopita Jiji Dar ES Salaam nchini Tanzania.
Bingwa huyo mara mbili wa mashindano ya baraza la ndondi duniani kwa sasa ni kati ya mabondia watatu wakike wa hapa nchini Kenya ambao washawahi kushinda ubingwa wa taji la shirikihso la ndondi pamoja na Conjestina Achieng pamoja na Sarah Achieng.
Zarika amekuwa na changamoto za udhamini baada ya mdhamini wake wa awali Sportpesa kujiondoa kutokana na sheria ngumu za ushuru wa serikali ya Kenya.

