VILABU VYA MALINDI VYALILIA BASI

Vilabu vya mashinani katika eneo bunge la Malindi vinazidi kulalamikia hali ngumu ya usafiri wanapoendesha ligi mbalimbali.

Mkufunzi Collins Omol ambaye anaiongoza klabu ya Yanga katika daraja la pili kitaifa amesema kwamba amesema kwa sasa usafiri unazidi kuwa kitendawili baada ya basi lililokuwa limenunuliwa na mbunge wa zamani wa Malindi Aisha Jumwa kuharibika.

Basi hilo limebaki katika gereji kwa miezi kadhaa hadi kufikia sasa huku kukiwa hakuna matumaini ya kufufuliwa.

Mkufunzi huyo sasa amenyoshea kidole cha lawama kwa ofisi na uongozi wa mbunge wa sasa katika eneo bunge la Malindi Amina Mnyazi kwa kukosa kusuluhisha matatizo ya wachezaji hao mashinani.