TOM JUMA APATA KAZI INGWE

Klabu ya AFC Leopards imempa kazi ya ukocha mkufunzi Tom Juma kuingoza klabu hiyo kwa kuchukua nafasi ya mkufunzi Patrick Aussems ambaye aliachana na majukumu ya kuiongoza klabu hiyo ya Ingwe.

Wakati uo huo Ingwe wamempa kazi za naibu mkufunzi Gred Ambani ambaye ni mcheaji wake wa zamani kusaidia na mkufunzi Tom Juma katika klabu hiyo.

Kamati kuu ya klabu hiyo ikiongozwa na Dan Shikanda iko na imani ya klabu hiyo kufanya vizuri msimu ujao chini ya uongozi mafundi hao wapya wa soka.

Patrick Auusems raia wa ujerumani alikataa kuongeza mkataba wake na mabingwa hao mara 12 kutokana na sababu zake binafsi baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa takriban miaka miwili na msimu uliopita kuifanya klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya 7 wakiwa na alama 51.