KAUNTI YA KILIFI KUREKEBISHA VIWANJA

Serikali ya kaunti ya kilifi inayoongozwa na gavana Gedion Maitha Mungaro inalenga kuanza urekebishaji wa viwanja vilivyoko mashinani mwa kaunti hiyo kama njia moja ya kuvipa hadhi ili kuruhusu wachezaji kuandaa mechi kwa ubora zaidi.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa katika mitandao rasmi ya serikali ya kaunti ni kuwa Ujenzi wa uwanja wa kisasa utasubiri kwa muda wanaporekebisha viwanja vilivyoko.

Ikumbukwe kwamba serikali hii baada ya kuingia uongozini iliahidi ujenzi wa kiwanja cha Water mjini Kilifi ambacho kinauwezo wa kuruhusu makuzi ya talanta mbalimbali.

Mungaro amesema kwamba uwanja huo utatamatika ndani ya kipindi cha miezi 18 ijayo.

Serikali ya kaunti ilitangaza kuwa wiki ijayo itakuwa inanunua basi jipya kwa vilabu vya mashinani, basi ambalo linauwezo wa kubeba watu 67.