Mechi ya kati ya klabu ya Inter Dabaso na Deep Sea jana ililazimika kutibuka baada ya kipindi cha kwanza kwa kile kinachotajwa kuwa mwenyeji ambaye ni Inter Dabaso alifeli kuzingatia za kuandaa mechi ya nyumbani baada ya kukosa kuwasilisha gari kwa ajili ya dharura kwa wakati unaofaa.
Akizungumza na Tama La Spoti mkufunzi wa Inter Dabaso klabu ya Watamu kaunti ya Kilifi anasema kwamba gari husika liliwasilishwa lakini mpinzani wao alikuwa amehizi kupoteza mechi hiyo baada ya kipindi cha kwanza kutamatika Inter Dabaso wakiwa mbele na mabao 2-0.
”Hao Deep Sea walikuwa wanaona wameshapoteza hiyo mechi wakatafuta vijisababu vingi. Gari tulileta na likatoka kiasi kuwekwa mafuta jamaa walipoona hakuna basi wakatoka tukiwa 2-0 mbele.” Alisema mkufunzi Sammy.
Kwa upande wa Deep Sea ni kuwa walifuata sheria za soka za daraja la pili na kukataa kurudi uwanjani baada ya mazungumzo na afisa mkuu wa mechi hiyo. Athman Pirezi ambaye ni mkufunzi wa Deep sea kutoka lamu anasema walichukua fusra hiyo ya kuchukua alama tatu baada ya mpinzani wao kufeli kutimiza sheria za fkf.
”Sisi tuliacha kucheza kwa kufuata sheria. Yawezekanaje tucheze bila gari ambalo lilifaa kutuhakikishia usalama. Tukaichukua kama advantage tuchukue alama tatu tuende zetu Lamu hata afisa wa mechi hiyo aliafiki.” Alijitetea Pirezi.

