Raphael Shigali ambaye ni bondia wa Kenya anaripotiwa kufariki dunia hapo jana kutokana na maandamano ya upinzani yalokuwa yanafanyika hapa nchini.
Taarifa zasema kwamba Shigali alipigwa risasi na mtu ambaye mpaka sasa hajabainika wakati wa maandamano yaliyokuwa yanahusisha wafuasi wa muungano wa upinzani Azimio la umoja na maafisa wa polisi jijini Nairobi alipokuwa anaelekea nyumbani kutoka kambi yake ya mazoezi.
Rahael Shigali ni bingwa wa mashindano ya Nairobi open Bantaweight na kufariki kwake kumeripotiwa na Jericho Boxing club iliyoko jijini Nairobi.
Shigali alikuwa kati ya mabondia waliosafiri kuelekea Mozambique jijini Maputo kwa mashindano ya mabondia wachanga mwaka 2022

