Mkufunzi wa klabu ya Samburu Lions Erick Muema ameachana rasmi na klabu hiyo ya kaunti ya Kwale.
Taarifa zasema kwamba ameamua kujiondoa kwa sababu zake binafsi baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa muda.
Huyo anakuwa mkufunzi wa hivi punde zaidi kuachana na klabu ya daraja la pili baada ya mkufunzi Nero Chishenga kuachana na furunzi mwezi mei pamoja na Peter Mole kuachana na klabu ya Beach Bay mwezi juni.
Ukata wa kifedha katika vilabu unazidi kukandamiza vilabu huku wakufunzi pamoja na baadhi ya wachezaji kukata tama ya kuendelea kushiriki michezoni kwa kukosa motisha.
Vilabu vingi ambavo havina udhamini mashinani vimekuwa vikililia serikali za ugatuzi kuja mashinani na kusaidia wachezajikujikwamua kutoka hali hiyo ngumu.

