Klabu ya Beach Bay kutoka eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, klabu inayoshiriki ligi ya daraja la pili kitaifa iko katika hatari ya kushuka daraja kutoka ligi hiyo kuungana na furunzi pamoja na klabu ya Maji Bombers kushuka daraja.
Beach Bay kufikia sasa imekosa kuheshimu ratiba mara mbili msimu huu kutokana na ukosefu wa usafiri hasa katika mechi za ugenini, moja dhidi ya Kishada fc na ya punde zaidi ni wikendi ilopita kukosa kusafiri kuelekea Mombasa kuvaana na Ziwani Youth.
Sheria ya ligi ya fkf katika daraja la pili ni kwamba timu itakayokosa kuheshimu ratiba mara moja katika msimu inafaa kushuka daraja.
wakati hayo yakijiri hii leo Ziwani Youth wanasafiri hadi shule ya msingi ya Makande mwendo wa saa tisa kuvaana na klabu ya Shimanzi fc wakati klabu ya kISHADA ikiratibiwa kucheza dhidi ya Samburu lions.
Kesho klabu ya Omax fc inayoongozwa na mkufunzi Juma Kalato wataikaikaribisha klabu ya Mariakani fc katika uwanja wa Ronald Ngala mjini Mombasa.

