RONALDO AINGIA KWENYE GUINNESS BOOK OF RECORDS

Mshambuliaji nguli wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo jana alizawadiwa cheti baada ya kuingia katika vitabu vya Guiness Book of Record kutokana na kucheza mechi nyingi zaidi akitumikia taifa lake.

Kwa sasa Ronaldo ndiye mchezaji pekee aliyewahi kufikisha mechi 200 kutumikia taifa baada ya kuanza kusakatia Ureno soka mwaka 2003.

Mreno huyo ambaye sasa ako na umri wa miaka 38 jana kwenye ushindi dhidi ya Iceland alifunga bao lake la 122 na kuwa mchezaji mwenye mabao mengi ya kimataifa.

Ronaldo ambaye sasa ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno pamoja na klabu yake ya Al Nassr ya Saudi Arabia Pro League ameshinda mataji ya Ballon DoR mara tano miongoni mwa matuzo mengine makubwa Ulaya.