Klabu ya Mathare United katika ligi kuu ya Fkf imethibitika Kushuka daraja hadi National Super League kuelekea msimu ujao.
Hii ni baada ya klabu hiyo kuandikisha matokeo duni msimu huu. Bingwa ligi ya Fkf msimu huu atabainika siku ya jumapili kutokana na Gor Mahia kupigwa na Homeboyz pamoja na Tusker kupiga sare na klabu ya Posta Rangers.
Kufikia sasa kumesalia mechi moja na Gor Mahia wanaongoza ligi na alama 67 huku Tusker ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wakisimama katika nafasi ya pili na alama 66.
Mshindi wa kombe msimu huu atakuwa bila hela baada ya shirikisho lasoka la fkf kutangaza kwamba msimu huu hawana hela za kutuza mabingwa kutokana na changamoto za ukosefu wa mgao wa pesa kupitia udhamini pamoja na masuala mengine.

