Aliyekuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya raga Paul Odera wa kikosi cha wachezaji 15 kila upande anasema kwamba timu ya taifa ya Kenya Shujaa ya wachezaji 7 kila upande ina uwezo wa kurudi katika raga za ngazi za juu licha ya kushushwa daraja mwezi Mei.
Mkufunzi Odera ambaye alichezea timu ya taifa ya Kenya miaka ya 90 pamoja na kuwa nahodha wa timu 2001 anasema kwamba Kenya inatalanta nyingi sana inaweza kurudi katika haliyake ya sawa iwapo serikali itawekeza vilivyo katika mchezo.
”Kusema ukweli hapa Kenya kuna talanta chungu nzima za raga. Cha kufanyika ni serikali ifanye uwekezaji ufaao kuitengeneza na kuvutia wachezaji wengi zaidi. Kuna makosa ambayo yalifanyika mpaka timu ya Kenya Shujaa ikashuka daraja lakini kitendawili hicho huenda kikateguliwa iwapo makosa yatarekebishwa. Kwa kweli Shujaa kushuka daraja sio kitu cha kuvutia mtu yeyote anayependa raga ya taifa hili.”
Mwezi Mei Kenya Sevens walishuka daraja baada ya kutandikwa na timu ya taifa ya Canada kichapo cha alama 12-7 na kuagana na raga za dunia tangia kuingia kwa mara ya kwanza mwaka 2003

