ZINDUENI TIMU ZA KINADADA – CORAZONE VIVIAN

Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Harambe Starlets Corazone Vivian  ambaye yupo nchini kwa likizo kutoka klabu yake ya sasa Simba Starlets iliyoko nchini Tanzania ametoa wito kwa  viongozi wa vilabu vya hapa nchini kubuni mbinu za kuanzisha vilabu vya kinadada ili kuifanya michezo kuwa na nafasi sawa kwa jinsia zote tofauti na ilivyo kwa sasa.

Amesema hatua hiyo itarahisisha vilabu vya kinadada kupata misaada tofauti na wenyewe kujitegemea wakiwa mashinani.

Corazon amesema kuwa mbali na sheria ya CAF kusema kwamba, vilabu vinavyofuzu kuingia mashindano ya shirikisho hilo vinafaa kuwa na vilabu vya kinadada, ni sharti wakuu wa vilabu wenyewe wachukue jukumu la kuunda timu hizo kama njia moja ya kukuza mchezo wa soka kwa kinadada.

Ametolea mfano taifa jirani la Tanzania ambalo vilabu  vikubwa vya wanaume kama vile  Simba na Yanga