Mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa ya Harambe Stars mwite Jacob Ghost Mulee amesistiza kwamba kuna umuhimu mkubwa wa shule za hapa nchini hasa katika shule za msingi kuanzisha mafunzo ya michezo mbalimbali ili makuzi ya talanta kuanza mapema.
Amesema kwamba nyota nyingi za wachezaji waliokuwa na uwezo wa kupeperusha bendera ya Kenya katika michezo kimataifa hufifia kisa kukosa makuzi asili ya mapema wakiwa na umri mchanga.
Ametoa wito kwa wabunifu wa mtaala wa elimu kuanzisha mikakati ya kuifanya michezo kuwa moja ya kipaumbele cha mafunzo kwa wanafunzi tofauti na ilivyo kwa sasa mbapo elimu ya kutafuta stakabadhi za kazi za kiofisi imepewa kipaumbele.
” Wale ambao ni watunzi wa mitaala ya elimu sasa wanafaa kuliangalia hili la kubuni mafunzo ya michezo zaidi na kutengeneza ‘academy’ ili watoto wetu waelewe michezo zaidi. Tukifanya hivyo tunauwezo wa kuzidua talanta zaidi ili kutangaza kenya kupitia vipaji vyetu. Malezi ya vipaji kutoka utotoni ni muhimu sana, hata mataifa yaliyoendelea yanafanya hivyo.”

