Klabu ya Kishada fc imepewa alama tatu na shirikisho la soka baada ya malalamishi kwamba klabu ya Beach Bay walikosa kuwasilisha maafisa wa polisi wa kutosha katika mechi yao katika shule ya msingi ya Mjanaheri Magarini kaunti ya kilifi.
Kulingana na FKF ni kwamba Beach Bay klabu inayoongozwa na mkufunzi Peter Mole ilihalifu sheria za soka kwa kukosa kuwasilisha maafisa wa kutosha kulinda usalama wakati wa mechi.
Clara Kadzo ambaye ni mweka hazina wa klabu hiyo awali alikuwa ameambia Tama la Spoti kwamba afisa huyo alikosa kufika uwanjani kwa muda kutokana na dharura baada ya kupata ajali.
Mechi hiyo ilitibuka kabla kuanza kwa kipindi cha pili pale klabu ya Kishada walipogoma kuingia kiwanjani kutokana na hofu ya usalama wao walipokosa hakikisho ya kuwepo kwa maafisa wa polisi.

