Messi amekubali kuhamia marekani katika Major League Soccer kwenye klabu ya Inter Miami akimaliza tetesi za uhamisho kuelekea Saudi Arabia au kurejea klabu ya Barcelona nchini Uhispania.
Messi raia wa Argentina ambaye atakuwa anafikisha miaka 36 mwezi ujao amekubaliana na uongozi wa klabu ya Inter Miami ambayo kwa asilimia kubwa inamilikiwa na David Beckham mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza.
Kilichobaki ni mkataba rasmi kufanikishwa na Messi kwenda chezea soka lake marekani kulingana na klabu ya Inter Miami.
Mshindi huyo wa kombe la dunia amesema kwamba angependelea kwenda kucheza marekani ambako ana mapenzi nako kuliko kwenda saka hela za Saudi Arabia ambako amepea ofa nono.
”Mimi singalii sana masuala ya pesa, Saudi Arabia nimepewa ofa nono lakini haina haja ya kusema nasaka pesa sana nisahau mapenzi yangu ya soka. Nataka kusema wazi hapa kwamba mimi naelekea Marekani kwa sababu mimi ni mpenzi wa soka kuliko hela zake.” Alisema Messi.
Kufuatia ushindi wake wa kombe la dunia Messi sasa anasimama katika nafasi nzuri ya kushinda taji la Ballon DOR mwaka huu licha ya kutofanya vyema sana katika mashindano ya klabu bingwa ulaya na klabu ya PSG.

