SANGO NI TIMU YA MASHABIKI

Klabu ya Sango Sportif katika ligi ya daraja la pili kitaifa inaandikisha matokeo mazuri msimu huu kutokana na ushabiki kindakindaki kutoka kwa mashabiki wao.

Klabu hiyo ambayo ni klabu ya pekee kucheza ligi kubwa kutoka kaunti ya Tana River inasimama katika nafasi ya nane kwenye msimu wao wa kwanza katika ligi hiyo baada ya kupanda daraja msimu uliopita kutoka ligi ya mkoa.

Kulingana na mkufunzi mkuu wa klabu hiyo Righo Jillo ni kwamba kuna uhusiano mzuri kati ya viongozi, wachezaji pamoja na mashabiki hivyo klabu inapata nguvu ya kusonga mbele.

”Hii ni timu ya mashabiki. Sanasana kila mtu anahusika katika kupeana mchango wake kwa klabu hii na tuko na utangamano mzuri. Mashabiki wetu ni watu wanapenda hii klabu kwa dhati ndio maana wanajitokeza katika mechi sana ili kuipa kasi klabu hii. Sisi hufanya vitu kwa pamoja.” Alisema Jillo.