KOKANE HUENDA AKAJIPATA MATATANI

Adhabu kali zaidi huenda ikamkuta Kokane Lango ambaye ni kipa wa klabu ya Sango Sportiff (kutoka Tana River) inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa kufuatia cheche za maneno aliyoyatoa kwa msimamizi wa mechi yao wikendi ilopita.

Katika mechi hiyo dhidi ya klabu ya Aston Rangers Lango alipewa kadi nyekundu kufuatia kumpiga mchezaji wa klabu ya Ashton Rangers jambo ambalo lilimchukiza refa wa katikati ya Uwanja na kufuata sheria ambayo ilimlazimu kumpa adhabu.

Taarifa zaidi zasema kwamba mchezaji huyo amekuwa na tabia ya kuzua vurugu katika mechi kadhaa za awali jambo ambalo limekuwa likikashifiwa kwenye soka na shirikisho la soka FKF.