HARAMBEE STARLETS KUKOSA OLIMPIKI

Timu ya taifa ya kinadada Harambe Starslets watakosa kushiriki mashindano ya soka ya olimpiki mwaka 2024 kutokana na marufuku ya fifa iliyochelewa kuondolewa mwaka jana.

Kulingana na afisa wa mawasiliano wa shirikihso la soka la FKF Ken Okaka amethibitisha kwamba Harambe Starlets Kenye ilichelewa kujisajili kutokana na marufuku iliyokuwepo.

Kenya pia ilitolewa katika orodha ya mataifa 25 ya shirikisho la soka barani Africa CAF ya kwenda Cairo mwaka huu kungangania nafasi mbili za mwisho  angalau kupata tikiti ya kushiriki mashindano hayo ya olimpiki.