Vilabu vya kaunti ya Kilifi vinalalamikia maonevu kutoka kwa marefa wa daraja la pili wanaposhiriki mechi dhidi ya vilabu vya Mombasa.
Kulingana na mkufunzi Peter Mole pamoja na mkufunzi wa klabu ya Inter Dabaso Coach Sammy ni kwamba vilabu vya Mombasa vinapendelewa sana na marefa.
Wakufunzi wa vilabu hivyo vya Kilifi wanazidi kutoa wito kwa shirikisho la soka kuhakikisha kuna usawa katika kuendesha msimu ili vilabu vingine visikate tamaa.
Kwa sasa vilabu kadhaa vinalalamikia gharama ya juu ya uendeshaji wa ligi wakisema kwamba ukosefu wa usawa pamoja na ufisadi wakati wa mechi unawakatisha tamaa ikizingatiwa hela ndefu wanazotumia katika msimu mzima.

