WAZIRI WA MICHEZO ASHAURI WACHEZAJI KUWEKEZA

Shirikisho la riadha nchini Kenya pamoja na wizara ya michezo linalenga kuanzisha mradi wa pensheni kwa wanariadha wa Kenya ili kuwakinga na njaa baada ya kustaafu.

Kulingana na waziri Ababu ni kwamba wachezaji wa Kenya wanafaa kuwa makini na kuwekeza hela wanazoshika wakiwa bado wanacheza ili kutofedheheka na umaskini uzeeni.

Ababu aliambia wanariadha na wachezaji wote kwa jumla kutambua kwamba tasnia hiyo ya michezo si ya muda mrefu hivyo kuwashauri kutumia muda wao pamoja na hela umakini kwani, kweli wachezaji hao hushika hela ndefu ndefu katika Mashindano hasa kimataifa.