Mkufunzi wa timu ya taifa ya Harambe Stars Engin Firat ameweka wazi kikosi chake atakachotumia katika mashindano yajayo ya mataifa manne pekee yatakayoanza rasmi tarehe 11 hadi 18 mwezi Juni.
Kikosi hicho cha wachezaji 30 kinachojumuisha wachezaji kutoka ligi ya Kenya na ligi za kigeni kitaanza rasmi mazoezi yake tarehe 5 mwezi ujao.
Kikosi kilichotambuliwa ni;
MAKIPA
Ian Otieno (Zesco, Zambia), Bryne Odhiambo (KCB) ,Brian Bwire (Tusker), Simon Masaka (Sofapaka)
WALINZI
Joseph Okumu (Gent, Belgium), Daniel Anyembe (Viborg, Denmark), Eric Ouma (AIK, Sweden) Collins Shichenje (KUPS), Daniel Sakari (Tusker), David Ochieng (Kenya Police), Abud Omar (Kenya Police), Mohamed Siraj (Bandari), Kevin Luke Otiala (Kariobangi Sharks), Robinson Kamura (Kakamega Homeboyz)
VIUNGO
Amos Nondi (Ararat, Armenia), Richard Odada (Philadelphia Union, USA), Kenneth Muguna (Azam, Tanzania), Teddy Akumu (Sagan Tosu, Japan), Alvin Mangeni (Kenya Police), Clifton Miheso (Kenya Police), Charles Ouma (Kenya Police), Abdallah Hassan (Bandari), Joseph Mwangi (Nzoia Sugar), Alpha Onyango (Gor Mahia), Bonface Omondi- (Gor Mahia), Victor Omune (AFC Leopards ).
WASHAMBULIZI
Michael Olunga (Al Duhail, Qatar), Masoud Juma (Difaa El Jadidi, Morocco), Moses Shummah (Kakamega Homeboyz), and Benson Omalla (Gor Mahia).
Harambe stars wanatarajiwa kushindania ubingwa wa mashindano hayo dhidi ya Mauritious ambao ni wenyeji wa mashindano, timu ya taifa ya Djibouti pamoja na timu ya taifa ya Pakistan.

