VIHIGA QUEENS WASHINDA MILIONI MOJA PEKEE BAADA YA KUPAMBANA LIGINI MIEZI TISA

Klabu ya Vihiga Queens ndio mabingwa wa ligi ya kinadada hapa nchini Kenya baada ya kuwa na kiwango kizuri sana msimu huu.

katika mechi yao ya mwisho iliyochezwa wikendi hii malkia hao wa Vihiga walisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gaspo Women.

Kabla ya ushindi huo Vihiga walikuwa wametangazwa mabingwa wa ligi hiyo kwani walikuwa mbele na alama nne tofauti na Gaspo waliokuwa na alama 48 kabla ya mechi ya siku ya Jumamosi.

kutokana na ushindi huo sasa Vihiga wamezawadiwa shilingi milioni moja, fedha ambazo zimekuwa zikikashifiwa kwa kile kinachotajwa kufeli kwa shirikisho.

Ligi ya wanaume inaelekea kutamatika na kulingana na rais wa shirikisho la soka FKF Nick Mwendwa, hakuna hela atakazopewa mshindi wa kombe la ligi kuu ya fkf.