MPISHI WA KENYA AACHANA NA ARSENAL UINGEREZA

Mkenya Bernice Kariuki ambaye amekuwa mpishi katika kambi ya Emirates kwa klabu ya Arsenal tangia mwaka 2020 amethibitisha rasmi kuachana na klabu hiyo.

Raia huyo wa taifa la Kenya mwenye umri wa miaka 51 ambaye alianza kama mpishi binafsi wa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal ambaye sasa ni mali ya Chelsea Pieer Emerick Aubameyang amethibitisha hayo kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook.

”Nashukuru uongozi wa klabu hii ya Gunners ambayo ni klabu kubwa ulimwenguni kwa kunipa kazi na kubwa zaidi asante kwa mashabiki wa klabu hii hasa wakenya. Ni muda wangu sasa wakuagana na klabu hii na kuenda kwengine. Nashukuru sana kwa kupata nafasi ya kufanya kazi hapa”, alisema Bernice

Bernice anaungana na baadhi ya wachezaji wanaoagana rasmi na klabu hiyo akiwemo Granit Xhaka ambaye atakuwa anayoyomea nchini ujerumani kucheza chini ya Xabi Alonso katika klabu ya Bayer Levarkusen.

Mpishi huyo (Bernice) ameshukuru uongozi wa The Gunners kwa kumpa kazi kwa kipindi cha miaka mitatu pamoja na mashabiki hasa wa kikenya kwa kuishabikia klabu hiyo pamoja naye.