HAALAND ASHINDA TUZO UINGEREZA

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City lakini pia timu ya taifa ya Norway Erling Braut Haaland amechaguliwa na kupewa tuzo la mchezaji bora wa mwaka 2023 wa muungano wa waandishi wa habari.

Haaland amepewa tuzo hilo kutokana na kuwa na kiwango bora msimu huu kwani katika msimu wake wa kwanza akiwa Manchester City amefunga mabao zaidi ya 51, mabao 36 ya ligi kuu nchini Uingereza yaliyosaidia klabu yake kubeba ubingwa wa ligi pamoja na mabao 12 ya klabu bingwa Ulaya ambako Manchester City kwa mara nyingine imepata nafasi ya kucheza fainali za Uefa.

Haaland pia ameshinda tuzo la mchezaji mataji mengine yakiwemo ligi kuu ya Uingereza, taji la kiatu cha dhahabu kwa kufunga mabao 36 ya ligi pamoja na kupewa tuzo la mchezaji bora mchanga ligini.

Pamoja na mafanikio mengine aliyokuwa nayo ligini msimu huu, Haaland ameingia na timu yake Manchester City katika fainali ya UEFA pamoja na fainali ya kombe la FA ambako anatarajiwa kuvaana na Manchester United.