BORUSSIA YANYATIA UBINGWA WA BUNDESLIGA HUKU BAYERN IKIMEZA MATE TU!

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Borrussia Dortmund kule Ujerumani mwite Edin Terzic anasema kwamba kurudi kwa Sebastian Haller baada ya kufanyiwa upasuaji ndio jambo linalozidi kuwapa Matumaini ya kunyanyua ubingwa wa Bundesliga msimu huu.

Katika mechi ya jana Sebastian Haller ambaye ni raia wa Ivory Coast alipachika mabao mawili wavuni mabao yaliyosaidia kuipa Borrussia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya klabu ya Ausberge.

Kwa sasa Borrussia wamesonga kileleni kwa ligi huku wakiwa wamesalia na ushindi mmoja pekee kuipokonya Bayern Munich ubingwa wa Bundesliga.

Kufuatia kichapo cha mabao 3-1 walichopigwa Bayern Munich na RB Leipzig sasa Borrussia wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 70 huku Bayern wakimezea mate Bundesliga waliwa na alama 68, mechi za mwisho za ligi zikitarajiwa kuwa zaidi ya fainali kwa wawili hao.