MANCHESTER CITY YASHINDA UBINGWA, KYLE WALKER AKITISHIA MASHETANI WEKUNDU

Klabu ya Manchester City ndio mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu 2022/2023 baada ya kusajili matokeo mazuri msimu huu.

Licha ya kushinda 1-0 dhidi ya Chelsea katika mechi ya jana (Jumapili) Manchester City inayoongozwa na mkufunzi Pep Guardiola ilikuwa imetangazwa mabingwa baada ya washika mtutu wa London Arsenal kupoteza kwa Nottingham Forest 1-0.

Beki wa kulia katika klabu ya Manchester City Kyle Walker ametuma onyo kwa Manchester United kwamba watawanyanyanganya ubingwa wa kombe la FA msimu huu.

Walker ameyasema hayo baada ya Manchester City kutawazwa mabingwa wa kombe la ligi kuu nchini Uingereza kwa mara ya tatu mfululizo.

Huo ni ubingwa wa tano katika historia ya Manchester City kushinda ligi kuu nchini Uingereza licha ya kuwa na safari ndefu msimu huu. Kongole