SOKA LA KILIFI LARINDIMA WIKENDI

Klabu ya Majenjeni Elite inayoongozwa na mkufunzi Emmanuel Kazungu jana ilizidi kujimarisha uongozi wake katika ligi ya eneo bunge la magarini katika chungu B baada ya kusajili ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kapupuni FC.

Kufikia sasa Majenjeni Elite wanaongoza ligi wakiwa na alama 25 baada ya kucheza mechi tisamatokeo mengine ya chungu hicho ni kwamba Uhuru fc walisajili ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Masuster FC huku Tabasamu fc wakipiga sare ya bao 1-1 dhidi ya Super Eagles.

Katika chungu A ni kwamba Sogorosa walisajili ushindi wa ugenini dhidi ya Whitestars kwa goli 1-0 huku Hope FC ikipigwa katika dimba lao la nyumbani kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Yanga. Wanafainali wa mashindano ya hivi majuzi ya Emirates Cup waite Venus fc walisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fila na hatimaye Kitwatani wakisajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Napoli.

Katika ligi ya eneo bunge la Kilifi kaskazini ni kwamba mabao mawili ya Mohamed Ibrahim pamoja na bao moja la Safari Kalama ndio mabao yaliyotosha kuwapa ushindi wa mabao 3-0 vijana wa Mkangagani fc dhidi ya klabu ya anzazi fc.Two stars fc na Bofa Youth walipiga sare ya bao 1-1 na hatimaye Racing Stars 1-1 na klabu ya Young Stars.