MASHINDANO YA KYISA MAKALA YA TISA KUFANYIKA KILIFI

Mashindano ya Kenya Youth Inter county Sports makala ya 9 ambayo yatafanyika mwaka ujao sasa yatafanyika katika kaunti ya Kilifi baada ya haya ya mwaka huu yanayoendelea katika kaunti ya Tharaka Nithi.

Ni kauli ya wizara ya michezo kupitia waziri Ababu Namwamba ambaye amekuwa akizungumza na vikosi vya kaunti mbalimbali jioni ya leo katika kambi ambayo timu zote zimekongamana kwa matayarisho ya mashindano hayo ambayo yanaanza rasmi kesho.

Kutokana na swala hilo sasa mkufunzi ambaye anaongoza kikosi cha kaunti ya Kilifi, Rio Ngumbao ambaye ni mkufunzi wa zamani wa klabu ya Kilifi Gold anasema kwamba kwa sasa ipo haja ya kaunti hii kuanza ujenzi wa viwanja ili kujitayarisha kwa ajili ya mashindano hayo.

Pamoja na hayo Coach Rio ametuma wito kwa wakuu wa vilabu vya kaunti ya kilifi kuanza kukuza vipaji vya wachezaji watakaowakilisha kaunti hii katika mashindano hayo mwakani.

Makala ya mwaka huu kule Tharaka Nithi yanalengwa kutamatika wikendi ijayo siku ya jumamosi na kuna zawadi ambazo zinatarajiwa kupewa washindi wa mwaka huu ambazo mbali na mataji na medali mkufunzi Rio anasema kuna hela kwa timu zitakazoibuka na ushindi.