Timu ya soka ya wanaume inayoongozwa na mkufunzi Rio Ngumbao imesajili sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Mandera katika mechi ya kwa nza kabisa iliyochezwa asubui ya leo.
Timu ya kilifi kwa upande wa kinadada inayoongozwa na mkufunzi Fathime Tibu imetandikwa kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya timu ya Tharaka Nithi ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo.
Katika mcheza wa mpira wa wavu timu ya kaunti ya Kilifi imesajili ushindi wa seti 3-0 dhidi ya timu ya kaunti ya Embu.
Mashindano haya yameanza rasmi hii leo na yataendelea hadi siku ya Jumamosi ambapo fainali za kuwania ubingwa wa makala haya ya nane ya kitaifa yatakuwa yanafanyika.

