KIKOSI CHA KILIFI CHAWASILI MLIMA KENYA

Kikosi cha kaunti ya kilifi kitakachowakilisha kaunti hii katika michezo ya Kenya Youth Inter County Sports Association mashindano yatakayofanyika kaunti ya Tharaka Nithi kiliwasili rasmi katika kaunti hiyo.

Kikosi hicho kimeundwa na wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 na wanajenga vikosi viwilivya soka ya wanaume na kinadada lakini pia kikosi cha akina dada katika mchezo wa mpira wa wavu.

Timu hiyo ya kaunti ya kilifi imekuwa ikipiga kambi mjini kilifi kwa mazoezi ya lala salama na kulingana na wizara ya vijana na michezo inayoongozwa na Mheshimiwa Dama Masha ni kwamba matumaini yapo kwamba watawakilisha kaunti hii kwa kusajili matokeo mazuri.

Mashindano haya ambayo ni makala ya 8 kilifi imepangwa katika kundi C kwenye soka pamoja na timu ya Homa Bay, Mandera, Wajir lakini pia kaunti ya Meru katika upande wa soka.

Kwenye soka la kinadada Kilifi imewekwa katika kundi la wenyeji Tharaka Nithi lakini pia kaunti ya Nyandarua na hatimaye katika mashindano ya mira wa wavu wanadada wa kaunti ya kilifi wamewekwa katika chungu kimoja na Tharaka Nithi, Busia, Uasin Gishu lakini pia kaunti ya Embu.