Klabu ya Liverpool usiku wa leo iakuwa inasafiri hadi dimba la Elland road kuvaana na Leeds United katika mechi ya ligi kuu nchini Uingereza saa nne usiku wa leo.
Mkufunzi wa Liverpool Jergen Klopp amethibitisha kwamba Luis Diaz ni kati ya wachezaji watakaowakilisha wekundu hao wa Mersisyde baada ya Mkolombia huyo kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na jeraha.
Klopp pia amesema kwamba anamatumaini makubwa ya kumaliza msimu huu vyema licha ya kuwa na matokeo mabaya katikati ya msimu hali ambayo imepelekea kuwa na wasiwasi wa kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya.
Kwa sasa Liverpool wanasimama katika nafasi ya nane wakiwa na alama 44 msimu huu.

