WEKENI SHERIA KALI, FKF YASHAURI

Wito umetolewa kwa bunge la kitaifa kuunda sheria za kuadhibu vikali washtakiwa wa upangaji wa matokeo pindi tu yanapotokea ili kupunguza kuwepo kwa matukio kama hayo katika siku za usoni kwenye ligi za hapa nchini.

Maafisa wa FKF wakiongozwa na Nick Mwenda leo wamekutana na kamati ya michezo na utamaduni na kuwasilisha hoja hiyo wakisema inahitaji kushughulikiwa mara moja.

Amesema wamekuwa wakiwasilisha kesi nyingi kortini kushtaki waasi wa sheria za upangaji wa matokeo lakini wamekuwa wakiachiliwa kutokana na kuwa kwa sasa hakuna sheria madhubuti za kuwahukumu vikali.

Pia ameeleza kuwa uhaba wa fedha katika shirikisho la soka na vilabu umekuwa ukichangia wasimamizi wa mechi wakihusika katika suala zima la upangaji wa matokeo.

Hii inatokana na hongo za mara kwa mara kwa baadhi ya marefa lakini pia wachezaji na tukio kubwa zaidi ni la hivi punde ambapo washtakiwa watatu walikamatwa na maafisa wa polisi walipokuwa wanapanga mechi ya Nairobi City Stars mwezi Machi tarehe 13.