Masuster ndio mabingwa wa mashindano ya Emirates Cup yaliokuwa yanafanyika wikendi hii katika uwanja wa Kaembeni, eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
Masuster Walishinda ubingwa huo kwa kuitandika Venus Fc kichapo cha mabao 2-0.
Mabingwa hao Walishinda elfu kumi pesa taslimu pamoja na sare ya soka lakini pia mpira huku nafasi ya pili akijishindia sare za mpira pamoja na mpira huku vilabu vyote nane vikipokea mpira kila mmoja.
Yalikuwa mashindano ya kurudishia jamii mkono wa shukrani na Frankline Amani ambaye ndiye mdhamini mkuu wa mashindano hayo.

