klabu ya Beach Bay imesajili ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya klabu ya Yanga FC inayongozwa na mkufunzi Collins Omol katika dabi ya kaunti ya kilifi iliyofanyika mchana wa leo katika uwanja wa mjanaheri, eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
mechi hiyo ilifaa kufanyika wikendi ilopita siku ya jumapili lakini ikalazimika kuahirishwa kutokana na klabu ya Yanga fc kutuma ombi kwa FKF kuahirisha mechi hiyo hadi leo kutokana na Yanga kushiriki katika masuala ya michango ya kugharamikia mazishi ya wachezaji wao watatu walifariki dunia kutokana na ajali ya barabarani iliyohusisha basi la chuo kikuu cha Pwani lililokuwa linaelekea kaunti ya Nakuru kwa michezo ya wanavyuo.
Kulingana na mkufunzi Collins Omol ni kwamba kwa sasa maandalizi ya mazishi yanaendelea na huenda wakaanza kusafiri jumalijalo kwa mazishi ya wachezaji ambao kwao ni bara mwa taifa hili la Kenya.

