Ferdinand Omanyala alianza msimu wake vyema kwa kutumia muda wa sekunde 10.12 katika mkondo wa kwanza wa Msururu wa ASA Grand Prix nchini Afrika Kusini.
Mwanariadha huyo mwenye kasi zaidi barani Africa aliongoza World Athletics Continental Tour kwenye Uwanja wa riadha wa Tuks mjini Pretoria Jumatano jioni.
Omanyala aliwapiku washiriki 7 wengine japo hakuweza kufanikiwa kukimbia chini ya mda wa sekunde 10.
Kinda wa raia wa Afrika Kusini, Benjamin Richardson aliibuka wa pili kwa muda wa sekunde 10.33, huku Roberts Rivaldo akimaliza wa tatu kwa sekunde 10.34.
Mkenya mwingine katika safu hiyo Samwel Imeta alimaliza wa nne kwa sekunde 10.39.
Omanyala alisema kwamba ushindi huo ulikuwa hatua kubwa kwake katika mwelekeo sahihi kwani unampa motisha zaidi kwenye harakati zake za kutafuta taji la dunia kwenye Mashindano ya Dunia huko Budapest.
DABI YA KAUNTI YA KILIFI HATIMAYE YARINDIMWA

