SADIO MANE APIGWA MARUFUKU NA KLABU YAKE

Klabu ya Bayern Munich imempiga marufuku Sadio Mane ya kutoshiriki mechi ya wikendi ijayo dhidi ya klabu ya Hoffeinhem katika uwanja wao wa nyumbani.

Marufuku hiyo inatokana na tukio la wiki hii ambapo Mane alimpiga ngumi mchezaji mwanzake Leroy Sane baada ya kupoteza mechi ya Uefa kwa mabao 3-0 dhidi ya klabu ya Manchester City.

Pamoja na adhabu ya marufuku Mane anatarajiwa kulipa faini kutokana na kumjeruhi Leroy Sane .

Baadhi ya wachezaji kambini mwa Allianz Arena washaanza kuzungumza kwamba tukio la Mane linaweza kumfanya kuwa na muda mfupi Bayern Munich na huenda akauzwa katika majira ya joto