Manchester City inayoongozwa na mkufunzi Pep Guardiola imetia guu moja ndani ya semi fainali za uefa msimu huu baada ya kusajili ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya klabu ya Bayern Munich Katika uwanja wao wa nyumbani Etihad.
Kiungo mhispania Rodri ndiye alikuwa wa kwanza kuifungia Manchester City kabla ya Bernado Silver kuitendea haki assist ya Halaand katika dakika ya 70 na hatimaye katika dakika ya 76 Halaand akafunga bao lake la 11 katika mashindano haya msimu huu.
Katika dimba la Estadio Da Luz ya kule Ureno ni kwamba Benfica wametandikwa na Inter Milan ya Italia kichapo cha mabao 2-0 . Nicolo Barella na Romelu Lukaku ndio wamesaidia klabu hiyo ya italia kufunga mabao yaliyopelekea kupata ushindi.

