Mkufunzi Collins Omol wa klabu ya Yanga FC amesema maombolezi pamoja na michango ya mazishi ya baadhi ya wachezaji wake waliokufa katika ajali mbaya ya barabarani walipokuwa wanasafiri na basi ya chuo cha pwani ndio chanzo cha kulazimishwa kuairishwa kwa mechi kati yao na Beach Bay kutofanyika siku ya jumapili wikendi ilopita.
Mechi hiyo sasa itafanyika kesho katika uwanja wa mjanaheri mwendo wa saa tisa za mchana. Mkufunzi Omol anasema kwamba bado wanaendeleza michango ya mazishi ya wachezaji hao watatu jambo ambalo lililazimu kutaarifu ofisi ya fkf kupewa muda zaidi ili kujitayarisha ikizingatiwa kwamba klabu hiyo inaandamwa na changamoto ya ukata wa kifedha.
Mkufunzi Omol ameelezwa kusikitishwa na ajali hiyo akisema kwamba imekuwa pigo kwa klabu yake pamoja na baadhi ya wachezaji kupoteza morali wanapongangana kuendeleza mashindano ya msimu huu katika ligi hiyo ya daraja la pili.

