Beki shoto wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza mwite Luke Shaw amesaini mkataba mpya utakaorefusha makazi yake kambini Old Trafford hadi mwaka 2027. Mkufunzi wake Erik Ten Hag amempongeza Shaw kwa chaguo hilo.
Kule Anfield ni kwamba Naby Keita atakuwa anaagana rasmi na Liverpool mwishoni mwa msimu huu kwa uhamisho usio kuwa wa malipo. Pamoja na Keita Oxlade Chamberlin lakini pia Arther Melo wa Brazil watakuwa wanatoka Liverpool mwishoni mwa msimu.
Wakati hayo yakijiri Liverpool usiku wa leo watakuwa safarini kuvaana na Chelsea katika dimba la Stamford Bridge mwendo wa saa nne usiku. BRIGHTON watakuwa ugenini kuvaana na Bournemouth wakati Leeds wakikipiga dhidi ya Nottingham Forest na hatimaye Leicester City watakuwa wanawakaribisha Aston Villa katika dimba la King Power.

