Mchezaji mkongwe katika klabu ya daraja la kwanza kitaifa nchini Kenya mwite Jumaa Shokoa sasa ameihama rasmi klabu ya Malindi Progressive na kujiunga na klabu ya Mombasa Omax Fc inayocheza ligi ya daraja la pili kitaifa.
Licha ya kwamba nguli huyo hajabainisha sababu rasmi ya kuigura Malindi Progressive ameushukuru uongozi wa mkufunzi Elly Katana kwa kumpa nafasi kusakata soka katika klabu hiyo
Mchezaji mwengine ambaye ameihama klabu ya Malindi Progressive hivi punde ni Jimmy Karisa ambaye kwa sasa haijabainika klabu rasmi ambayo amehamia.
Mbaruk Pascal, winga mwenye umri wa miaka 25 analenga kuachana na klabu yake ya Junda Strikers na kutafita hifadhi katika klabu nyingine. Kwa sasa hakuna klabu ambayo imeonyesha nia ya kuhitaji huduma zake katika dirisha la uhamisho la sasa.
Mbaruk ni mchezaji wa zamani wa vilabu kadhaa ikiwemo Sarigoi Youth inayocheza ligi ya mkoa, klabu ya B13 ya kisauni pamoja na klabu ya Black Santos inayocheza ligi kuu ya kaunti ya Kilifi.

