Mkufunzi mkuu wa klabu ya Yanga FC Collins Omol amemsuta vikali mkufunzi wa Furunzi FC Nero Chishenga kwa kile anachokitaja kwamba Nero alikosa kufuata sheria za michezo katika harakati za kuwasilisha lalama zake kuhusu mechi ya wikendi ilopita ambapo wawili hao walikutana katika uwanja wa Alaskan na mechi hiyo kutamatika kwa Yanga kuibuka washindi kwa mabao 4-1.
Nero amewasilisha lalama kwa fkf akisema kwamba Yanga fc walimchezesha Baraka Mramba maarufu kama Abila kinyume na sheria kwani mchezaji huyo si sajili rasmi ya Yanga.
Collins Omol ameshikilia kwamba Abila ni mchezaji wa Yanga na alikosa kumchezesha mchezaji huyo katika mechi dhidi ya Samburu Lions kutokana na masuala ya kinidhamu tu tofauti na madai ya mkufunzi Nero.
Kwa upande wake Nero ameshikilia kwamba hatasitisha harakati zake za kutafuta haki kwa shirikisho la soka la fkf na kwamba ako na taarifa rasmi kuwa Baraka Mramba maarufu kama Abila anasalia kuwa mali ya Samburu Lions tofauti na anavyosema Omol.

