TUTASHINDA MATAJI YOTE MSIMU HUU – KOGALO

Mkufunzi Johnnathan McKINSTRY wa klabu ya Gor Mahia anasema kwamba msimu huu vijana wake wanalenga kushinda mataji yote msimu huu.

Ameyazungumza hayo baada ya kusajili ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Vihiga Bullets wiki hii na kurefusha uongozi wao ligini hadi alama 6 dhidi ya wapili Tusker fc.

Katika ligi ya mashindano ya kombe la Mobbert Bet Kogalo wameingia katika hatua ya 16 na mkufunzi McKinstry anaimani kwamba mwaka huu watatawazwa mabingwa wa kombe hilo.