Mkufunzi wa klabu ya Samburu Lions, Erick Muema, maarufu kama Badizzo anasema kwamba ameridhishwa na vijana wake katika ligi hiyo ya daraja la pili kitaifa katika roundi ya kwanza ya mashindano hayo.
Hadi kufikia sasa klabu hiyo imepoteza mechi mbili pekee zote katika uwanja wao wa nyumbani kutokana na mechi 12 ambazo wameshiriki msimu huu.
Anasema kwa sasa Samburu Lions wanalenga kuandikisha matokeo mazuri katika roundi ya pili ya msimu huu wakilenga kupanda daraja la kwanza kitaifa mwishoni mwa msimu huu.

