HALAAND KUKOSA MECHI YA KESHO

Huenda mshambuliaji wa timu ya taifa ya Norway Erling Braut Halaand akakosekana katika mchuano wa ligi kuu ya Uingereza kesho dhidi ya klabu ya Liverpool.

mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amesema kwamba mchezaji huyo bado anaugulia jeraha ambalo alilipata hata kabla ya likizo ya mechi ya ligi, kuelekea kwa mashindano ya kutafuta tikiti ya kufuzu kwa mashindano ya mataifa ya Euro mwaka 2024.

Huenda hili likawa pigo kubwa kwa mkufunzi Pep Guardiola kwani Haaland amekuwa kiungo muhimu katika ushindi wa mechi nyingi za Manchster city kwani amefunga mabao 42 katika mechi 37 msimu huu.