FURUNZI FC KUFANYA MAJARIBIO YA WACHEZAJI WACHANGA

Klabu ya Furunzi fc inayochezea ligi ya daraja la pili kitaifa sasa imeanzisha mchakato wa kutafuta wachezaji ili kuongeza kasi katika kikosi hicho kuelekea roundi ya pili katika mashindano hayo.

Mkufunzi wa klabu hiyo Nero Chishenga anasema kwa sasa wanatafuta wachezaji walio na kati ya miaka 17-23 katika sehemu za ushambulizi, viungo pamoja na ulinzi.

Nero anasema kwamba hatua hiyo imetokana na wachezaji kadhaa tegemezi katika kikosi chake kuwachana na soka kutoka na masuala ya uchumi pamoja na wengine ambao ni wanafunzi kurudi shule.