SAMBURU LIONS YAICHAPA YANGA UGENINI

Klabu ya Samburu Lions jioni ya leo imesajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Yanga FC katika mechi ya daraja la pili kitaifa katika uwanja wa Alaskan mjini malindi kaunti ya Kilifi.

Samburu lions walilazimika kutoka chini na kusajili ushindi huo wa ugenini baada ya kupigwa bao moja katika kipindi cha kwanza.

Mkufunzi wa Samburu Lions mwite Erick Muema maarufu kama Baddizo wakati akizungumza na Tama La Spoti baada ya mechi anasema amefurahishwa sana na matokeo ya mechi hiyo kutokana na mabadiliko ya mfumo baada ya kipindi cha kwanza

Baddizo anasema kwamba matokeo hayo sasa yanawapa motisha vijana wake wa kuendelea kuwasha moto katika ligi hiyo wakilenga kupanda daraja la kwanza kitaifa msimu ujao.