Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Togo Emmanuel Adebayo ametangaza rasmi kusafu soka la ushindani baada ya kushiriki kabumbu hilo kwa kipindi cha miaka 22.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 anastafu soka akiwa amefunga mabao 97 ndani ya mechi 241 akiwa ligi kuu nchini uingereza ambako amechezea vilabu kadhaa ikiwemo Arsenal kuanzia mwaka 2006 aliposajiliwa kutoka Monaco na Arsen Wenger.
Adebayoh pia amechezea Real Madrid, Manchester City, Totenham Hotspers lakini pia Crystal Palace.

