Akina mama katika eneo bunge la Magarini kaunti ya KIlifi wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatembelea kliniki zilizoko karibu na makaazi yao, wiki sita baada ya wao kujifungua ili kupata huduma za kupanga uzazi.
Kwa mujibu wa afisa mkuu wa nyanjani katika eneo bunge hilo Florence Cherono,idadi kubwa ya akina mama wamekuwa wakisusia maagizo hayo, ambayo hutolewa na wauguzi kwa akina mama wanaojifungua watoto na hivyo kusababisha athari za kiafya kwa watoto na akina mama hao.
Akiwahutubia wakunga pamoja na akiana mama katika wadi ya Magarini eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, amesema kuwa licha ya dini kuwapatia akina mama uhuru wa kijifungua watoto wengi, ipo haja ya wao kuzaa kulingana na uwezo wao wa kifedha.
Wakati uo huo amewa sisitiza akina mama kuhakikisha kuwa wanaruhusu wanao kupewa chanjo ya HPV wanapokuwa shuleni, kwani inawasadia wasichana walio na umri wa kati ya miaka 10 -14, dhidi ya kupata maradhi ya saratani ya kizazi.
WANAWAKE WAJAWAZITO ENEO LA MAGARINI WATAKIWA KUFIKA KWENYE KLINIKO ZILIZOKO KARIBU NA MAKAZI YAO

