VIONGOZI WALIOKAMATWA WAKIANDAMANA KUFIKISHWA MAHAKAMANI SIKU YA ALHAMISI

Kiongozi wa wachache katika bunge la seneti ambaye na pia seneta wa kaunti ya Kilifi, Stewart Madzayo, mbunge Opiyo Wandayi, mbunge Amina Mnyazi, mbunge Ken Chonga wanatarajiwa kufika mahakamani siku ya Alhamisi.
Viongozi hao watajibu mashtaka ya kukusanyika pasipo kibali yani illegal assembly.
Hii ni baada ya wabunge hao kutiwa mbaroni mapema hapo jana kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 50
Aidha wabunge hao wamesema kuwa kamwe hawatishwi na mashtaka dhidi yao kwani wanachokipigania ni haki za kimsingi za wananchi